Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Marekani Donald Trump ametanga kwamba wanajeshi wa Marekani wataanza kuondoshwa nchini Syria na kurejeshwa nyumbani, kwavile wameshafanikiwa kulitokomeza kundi la kigaidi la Daesh au Dola la Kiislam (IS).
Uamuzi huo wa kuondoa kabisa wanajeshi wa Kimarekani nchini Syria, umethibitishwa pia na maafisa wa Marekani na unatarajiwa kutekelezwa katika miezi ijayo.
Kuondoka kwa majeshi ya Marekani nchini Syria kutapelekea Syria kupata amani ya kudumu.
Maseneta wakosoa uamuzi wa Trump
Uamuzi huo wa Trump umekosolewa na Maseneta pamoja na baadhi ya wanachama wenzake wa chama cha Republican, ambao wanadai kwamba kuondoka kutazipa nguvu Urusi na Iran, ambazo zinamuunga mkono Rais wa Syria Bashar Assad na kuidhoofisha Israel ambayo ndio msaada mkuu wa makundi pinzani. Maseneta hao wa Marekani ikiwa ni pamoja na wa chama cha Republican Jumatano usiku walimsisitizia Rais Donald Trump kutafakari upya uamuzi wake huo wa kuondoa majeshi ya Marekani kutoka Syria.
Makamanda wa jeshi la Marekani waliopo Syria, ambao wamekuwa na uhusiano mzuri na viongozi wa kundi la wapiganaji wa kikurd wameeleza wasiwasi wao juu ya uamuzi huo wa Trump na jinsi utakavyohatarisha vikosi vya magagaidi vinavyoungwa mkono na Marekani.
Lakini Trump amesema kwake yeye operesheni ya Syria imemalizika, kwavile wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesha wameshapoteza maeneo waliokuwa wakiyadhibiti.
Maafisa wa Marekani wamesema wanajeshi wataanza kuondolewa Syria katika siku 60 hadi 100 zijazo na kwamba Wizara ya Mambo ya Nje itaanza kuondoa wafanyakazi wake kutoka Syria katika kipindi cha masaa 24.
Ikumbukwe kuwa Marekani ilipeleka majeshi yake nchini Syria kwa kutumia nguvu na bila ridhaa ya serikali ya Syria.
Ambapo Iran na Urusi zimepeleka majeshi yao nchini Syria kwa maombi ya serikali.
Pia Marekani imetuhumiwa na wapelelezi wa Urusi kwa kuwatorosha viongozi wa magaidi na kuwapeleka Afghanstan.
Mwisho wa habari/ 291